HISTORIA YA ASASI YA UKOMBOZI WA VIJANA TANZANIA
(AUVITA)
Shirika hili limezishwa kutokana na ushiriki wa shughuli mbalimbali za Uhifadhi wa mazingira katika Chuo Kikuu Cha Stella Maris Mtwara (STEMMUCO) tangu mwaka 2011 chini ya klabu ya MALIHAI. Kutokana na shughuli hizo ndugu Simba Mramba alizua wazo la kuanzisha Klabu ya TAKUKURU ili kupata na kusambaza elimu ya Utawala bora na misingi ya maadili katika jamii mnamo tarehe 25/9/2012 hata hivyo kwa kushirikiana na wenzake walifanikiwa kuanzisha klabu hiyo chini ya ulezi wa Afisa TAKUKURU Mkoa ambaye pia wanashirikiana nae katika shughuli mbalimbali za klabu hiyo, hata hivyo wazo hili halikuishia hapo ndugu Simba Mramba alishauri elimu hii tuiendeleze katikaka jamii ya watanzania wote, wanachama wengine hawakusita kukubaliana na wazo hilo hivyo tukaamua kuanzisha ASASI YA UKOMBOZI WA VIJANA TANZANIA(AUVITA) kwa kushauriana na Afisa TAKUKURU Mkoa Mnamo Tarehe 22/9/2013 huku tukiwa na maono enderevu ya ustawi wa jamii ya watanzania kwa kuijenge jamii misimgi na uwezo wa kuyatambua matatizo ya KIMAZINGIRA, KIJAMII, KIUCHUMI NA KITEKNOLOJIA na mbinu za kuweza kupambana nayo. Kwa kushirikiana na Kitengo cha Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Mtwara Mjini tuliandaa KATIBA ya asasi na kufuata taratibu stahiki za kuisajiri na tukafanikiwa kusajiri.